±¬ÁϹ«Éç

Bloomberg, SEforAll announce plan to accelerate energy transition in developing countries

Get monthly
e-newsletter

Bloomberg, SEforAll announce plan to accelerate energy transition in developing countries

Michael Bloomberg and Damilola Ogunbiyi to expand partnership to mobilize financing for clean energy projects
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
7 Novemba 2022
President Akufo-Addo of Ghana, Mr. Bloomberg, Ms. Ogunbiyi and other guests at the announcement event.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 

Bilionea wa Marekani na mwanzilishi wa Bloomberg Philanthropies, Michael Bloomberg, na Afisa Mkuu Mtendaji na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote, ( - SEforAll),Ìý Damilola Ogunbiyi mnamo tarehe 7 Novemba 2022 walitangaza upanuzi wa ushirikiano wao ili kuhamasisha ufadhili wa mpito wa nishati katika mataifa yanayoendelea barani Afrika, Asia na Amerika Kusini.

Michael Bloomberg

Ni habari njema kutoka kwa COP27 huko Sharm El Sheikh, Misri, ambapo viongozi wa ulimwengu, sekta ya kibinafsi, wanaharakati wa tabianchi, na mashirika ya kiraia kwa sasa wanajadiliana kikamilifu kuhusu njia za kukabiliana na hatari ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kufikia lengo la kutozalisha hewa chafu kabisa ifikapo mwaka 2050.

Mkakati wa mielekeo miwili wa Bloomberg Philanthropies ni kushirikiana na serikali za kitaifa na za mitaa ili kuzisaidia kuendeleza mipango ya mpito wa nishati na kushirikiana na Ìý ili kukusanya mtaji kwa miradi ya nishati safi katika mataifa.

Bw. Bloomberg, ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Matarajio ya Tabianchi na Suluhu, alisema hatua zinahitajika katika kukomesha viwanda vya makaa ya mawe duniani kote, na akaongeza kuwa uhisani wake utapanua kazi yake ya kuendeleza nishati safi barani Afrika.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Bi. Ogunbiyi, na Waziri wa Mazingira wa Nijeria Mohamed Abdullahi walisisitiza haja ya mpito wa nishati ya haki na usawa kwa mataifa ya Afrika.

Ghana "itatumia fursa ya mpito wa nishati ya haki na usawa kwa wingi kwa ukuaji wa kiuchumi kwa kuwa taifa hilo linategemea viwanda vinavyotumia kaboni
Akufo-Addo
Ghana’s President

Mfumo wa mpito wa nishati wa Ghana

Ghana "itatumia fursa ya mpito wa nishati ya haki na usawa kwa wingi kwa ukuaji wa kiuchumi kwa kuwa taifa hilo linategemea viwanda vinavyotumia kaboni," alisema Rais Akufo-Addo. Aliufafanua Mfumo mpya wa Kitaifa wa Mpito wa Nishati wa Ghana () ÌýÌýambao utatumika kama mwongozo wa "kubadilisha Ghana kuwa taifa la nishati ya kaboni ya chini inayostahimili tabianchi."

Mfumo wa utekelezaji wa Ghana utakaoghalimu $ bilioni 562 utaendelea kutoka 2020 hadi 2070, ingawa unalenga kufikia upatikanaji wa nishati kwa wote ifikapo 2030.

Taifa hilo litaondoa kaboni katika sekta yake ya nishati kupitia teknolojia ya kuteka kaboni, utumiaji na uhifadhi. Aidha, itaongeza matumizi ya magari ya umeme na seli za mafuta ya haidrojeni na vifaa vya matumizi ya nishati kwa ufanisi.

Ghana pia inatarajia kuzalisha ufadhili kupitia ushirikiano na benki za ndani za maendeleo na uwekezaji, mifuko ya malipo ya uzeeni na taasisi nyingine za kimataifa za kifedha.

Tunautafuta "mpito wa haki na wa usawa katika upatikanaji wa umeme kwa wote na matumizi ya maliasili zetu kusaidia maendeleo ya kiuchumi," kwa mujibu wa Wizara ya Kawi wa Ghana.

Njia ya kutozalisha kabisa hewa hatari ni kulenga kutokomeza umaskini wa nishati, hasa katika bara langu la Afrika...ni lazima nishati, tabianchi na maendeleo yaandamane
Ms. Damilola Ogunbiyi
CEO and Special Representative of the UN Secretary-General for Sustainable Energy for All

Njia ya kutozalisha kabisa hewa hatari

Bi. Ogunbiyi alielezea msaada wa Blomberg Philanthropies kwa mpito wa nishati yenye haki na usawa kote barani Afrika na Asia kama uliofika kwa wakati ufaao.

"Njia ya kutozalisha kabisa hewa hatari ni kulenga kutokomeza umaskini wa nishati, hasa katika bara langu la Afrika," alisisitiza, akiongeza kuwa "ni lazima nishati, tabianchi na maendeleo yaandamane," alisema Bi. Ogunbiyi.

Ìý "Changamoto za muda mfupi lazima zishughulikiwe lakini sio kwa gharama ya uendelevu wa muda mrefu ... ni lazima $ bilioni 100 zilizoahidiwa na ulimwengu ulioendelea zitolewe."

Bi. Ogunbiyi aliipongeza Ghana kwa kuonyesha ari, kama mataifa mengine mengi yanayoendelea yalivyofanya, kwa kuendeleza na kutekeleza "mipango ya mpito wa nishati iliyokamilika, inayoendeshwa na data na inayoweza kuwekezwa."

Ghana inajiunga na orodha inayokua ya mataifa, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini na , zenye mipango ya mpito ya nishati ya haki.

Ili kutekeleza mipango ya mpito wa nishati kwa mafanikio,Ìý hata hivyo, Waziri wa Mazingira wa Nijeria Mohamed Abdullahi alisisitiza kwamba, lazima mataifa yanayohusika zaidi na utoaji wa hewa ya kaboni yachukue hatua za haraka na madhubuti ili kusaidia mataifa yanayochangia uzalishaji mdogo lakini yanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na hatari ya tabianchi.

Mada: