±¬ÁϹ«Éç

Kubadilisha Mifumo ya Chakula ya Afrika: changamoto na fursa

Get monthly
e-newsletter

Kubadilisha Mifumo ya Chakula ya Afrika: changamoto na fursa

— Mazungumzo na Ibrahim Mayaki, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika
Kingsley Ighobor
Afrika Upya: 
29 June 2023
©´¡»å´Ç²ú±ð³§³Ù´Ç³¦°ì
Kubadilisha Mifumo ya Chakula ya Afrika: changamoto na fursa.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti iko kwa Kiingereza.

Ibrahim Mayaki, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika wa Mifumo ya Chakula, hapo awali aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD). Kabla ya Mkutano wa Kutathmini Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa uliopangwa kufanyika mjini Roma tarehe 24 - 26 Julai 2023, Kingsley Ighobor kutoka Afrika Upya alimhoji Dk. Mayaki. Walijadili masuala mbalimbali kuhusu hali ya mifumo ya chakula barani Afrika na fursa na changamoto zinazohusika katika kulisha idadi ya watu inayokua kwa kasi. Yafuatayo ni madondoo kutoka kwa mazungumzo yao ya kufahamisha:

Ibrahim Mayaki, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika wa Mifumo ya Chakula, hapo awali aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD).

Kama Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika wa Mifumo ya Chakula, upeo wa mamlaka yako ni upi na Waafrika wanapaswa kutarajia nini kutoka kwako?

Jukumu la wajumbe maalum wa Umoja wa Afrika kimsingi ni kushughulikia suala muhimu ambalo Umoja wa Afrika unahitaji uungwaji mkono kwalo. Mjumbe maalum hachukui nafasi au kuchukua majukumu ya Umoja wa Afrika au Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC). Badala yake, jukumu langu ni kusaidia na kuimarisha kazi yangu kwa kuleta thamani ya ziada.

Hii ni mara ya kwanza kwa Umoja wa Afrika kuteua Mjumbe Maalum wa mifumo ya chakula. Hapo awali, watu mashuhuri kama vile Donald Kaberuka wa Rwanda aliwahi kuwa Mjumbe Maalum wa Ufadhili na Michel Sidibé kutoka Mali kama Mjumbe Maalum wa Shirika la Dawa la Afrika.

Kuna sababu tatu kuu zilizochangia uamuzi huu wa kuteua mjumbe maalum wa mifumo ya chakula. Masuala haya yalijadiliwa kwa kina nilipokubali kuteuliwa.

Kwanza, tunaweza kuingia enzi ya baada ya vita vya Ukraine ambayo itakumbwa na janga la mifumo ya chakula.

Soko limeshuhudia mageuzi yasiyofaa, na nchi za Afrika zinakumbwa na athari za vita hivyo. Tumeshuhudia uhaba wa rasilimali muhimu kama vile mbolea, mbegu, ngano n.k. Janga na mwitikio wetu kwa hilo umefichua ukosefu wa juhudi zilizoratibiwa.

Kwa hivyo, sababu ya kwanza ya kuteua Mjumbe Maalum ni kuhakikisha kujiandaa kwa janga kama hilo, hata tunapotarajia majanga zaidi katika siku zijazo.

Sababu ya pili inahusiana na mikakati mingi inayoshughulikia masuala ya mifumo ya chakula barani Afrika. Tuna utata fulani katika masuala ya mikakati, na utata huu unahitaji usimamizi bora na uwiano.

Bila uratibu unaofaa, Nchi Wanachama na wadau wao wanaweza kutatizika kuelewa kule tunakoelekea. Kwa hivyo, uteuzi huu unalenga kukuza utayari na kuongeza uwiano kati ya mikakati hii.

Sababu ya tatu, inayohusishwa kwa karibu na hizo mbili zilizopita, inahusu utafutaji wa rasilimali. Hasa, inarejelea haja ya kutafuta rasilimali za ndani kushughulikia changamoto zinazokabili mifumo ya chakula.

Pia tuna rasilimali za benki za maendeleo ya kimataifa na taasisi zingine ambazo zinaweza kusaidia juhudi za Afrika katika kubadilisha mifumo yake ya chakula.

Mbali na vita vya Ukraine, ni mambo gani mengine yanayohatarisha mifumo ya chakula barani Afrika?

Nitaanza kwa kufafanua dhana ya mifumo ya chakula. Hapo awali, na hata sasa, tumezungumza kuhusu kilimo, uzalishaji wa kilimo, uchumi wa vijijini, tija ya kilimo, usalama wa chakula na ukosefu wa usalama.

Tunazungumza kuhusu mifumo ya chakula sasa kwa sababu inajumuisha wigo mzima, kwa njia moja, ya michakato, kutoka kwa mkulima hadi kwa walaji, na, kati ya wahusika na sekta nyingi.

Ni wazi kuwa mifumo ya chakula inahusu uzalishaji, lishe, barabara na miundombinu mingine, masoko na biashara. Inahusu kuwaunganisha wakulima na masoko, kuhusu elimu na ujasiriamali, kuwezesha wakulima wadogo kuwa wajasiriamali wadogo. Inahusu kilimo biashara.

Zaidi ya hayo, inasisitiza umuhimu wa kuwapa watumiaji taarifa muhimu na kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi, hasa katika maeneo kama Afrika ambayo yanateseka sana licha ya kuwa na kutochangia gesi chafu.

Tukiitazama Afrika leo, ni kweli tumepunguza umaskini uliokithiri katika kipindi cha miaka 20 hadi 25 iliyopita, lakini wakati huohuo kuna ongezeko la utapiamlo.

Gharama yetu ya kuagiza chakula bado iko juu sana, zaidi ya dola za Marekani bilioni 60 kwa mwaka. Wakulima wadogo ambao wanazalisha asilimia 80 ya chakula tunachokula pia wanakumbwa na utapiamlo na uhaba wa chakula, jambo ambalo si la kawaida.

Tumetumia mifumo kama vile [Mpango Kamili wa Maendeleo ya Kilimo Afrika] na kushughulikia maendeleo ya kilimo. Azimio la Malabo linachukuliwa kuwa mtangulizi wa mifumo ya chakula kwa sababu liliweka kilimo wazi kwa sekta nyingine.

Kwa namna fulani ni awamu ya pili ya CAADP, na imetekelezwa vyema ambapo zaidi ya nchi 40 zimepitisha mipango ya kitaifa ya uwekezaji katika kilimo. Benki ya Maendeleo ya Afrika imeanza kuandaa mikataba katika ngazi ya kitaifa ili kuwezesha nchi kuwa na mifumo itakayovutia ufadhili.

Kwa hivyo, tunayo mifumo, lakini tunahitaji mambo mawili makubwa kutokea.

La kwanza ni kuwa na mtazamo wa serikali nzima kuelekea mabadiliko ya mifumo ya chakula na sio kuiachia wizara ya kilimo au mazingira.

La pili, tunahitaji kuwekeza zaidi katika mifumo ya chakula ili kupunguza uhaba wa chakula. Katika [iliyofanyika Aprili tarehe 28-30, 2023] nilisema kuwa uhaba wa chakula sio suala la uzalishaji; ni suala la umaskini. Mwishowe lengo kuu ni kupambana na umaskini.

Kuhusu CAADP, tunaona kwamba nchi nyingi bado hazifikii ahadi zao za kuwekeza asilimia 10 ya bajeti za kitaifa katika kilimo na maendeleo vijijini?



Vyema.Ìý Ni takribani nchi 10 hadi 12 tu kati yaÌý zaidi ya 50 zimeweza kufikia lengo la kuwekeza asilimia 10 ya bajeti zao za kitaifa katika kilimo.

Hata hivyo, baadhi ya nchi zinadai kufikia kiwango cha asilimia 10, lakini matumizi yao yanajumuisha vitu ambavyo havihusiani moja kwa moja na mifumo ya chakula au mabadiliko ya kilimo kupitia mpango uliounganishwa.

Unapokuwa na mkuu wa nchi ambaye anaweka kipaumbele katika mageuzi katika kilimo na kuweka shinikizo lanaloleta matokeo na athari, mageuzi hayo hutokea. Kwa hivyo, suala la uongozi ni muhimu.

Kiufundi, tunajua nini kinafaa kufanywa—mbinu za kilimo, upatikanaji wa soko na fedha, na kuongeza mavuno—lakini tunahitaji suluhisho la kisiasa na azma ya kusonga mbele.

Wakati mwingine unakuwa na uongozi unaofaa lakini unakosa mifumo muhimu. Viongozi lazima waanzishe mifumo na wahakikishe ufanisi wao katika kufikia matokeo yanayotarajiwa.

Je, unatarajiaje uwezekano wa AfCFTA [Eneo Huru la Biashara Barani Afrika] kuimarisha mifumo ya chakula barani Afrika, kwa kuzingatia matatizo na haja ya mtazamo jumuishi?

AfCFTA inalenga kutatua masuala ya vikwazo vya ushuru na visivyo vya ushuru na kuwezesha usafirishaji wa bidhaa na huduma. Hizi zinahitaji kufanyia kazi masuala ya utendakazi kama vile sheria na kanuni.

Lakini sio AfCFTA yenyewe ambayo itawezesha uzalishaji. Mafanikio ya AfCFTA katika kuboresha mageuzi ya mifumo yetu ya chakula yanategemea upatikanaji wa miundombinu imara kama vile barabara, reli na vifaa vya kuhifadhi chakula.

Kwa hivyo AfCFTA ni chombo muhimu, lakini lazima ijazwe na sera nzuri na miundombinu iliyoendelezwa vyema.

Je, hilo linaweza kufanywa?

Tena, nasisitiza umuhimu wa uongozi bora wa kitaifa katika kushughulikia changamoto zetu zilizopo, kwani nyingi zinahitaji suluhisho katika ngazi ya kitaifa. Ingawa suluhisho za kikanda ni muhimu, serikali za kitaifa zinahitaji kukumbatia na kutekeleza suluhisho hizi za kikanda.

Zaidi ya hayo, ni muhimu kuhakikisha uwiano kati ya mipango yetu yote. Hatupaswi kutumia mitazamo tofauti kutoka kwa taasisi mbalimbali, kwa kuwa huko kunaweza kujenga hali ya mipango ya ushindani. Badala yake, lazima tuweke mifumo yetu ya kimkakati na kuwahimiza washirika wetu kufuata mifumo hii.

Mifumo hii inajumuisha CAADP, Azimio la Malabo, na , ambao ulitengenezwa kupitia midahalo jumuishi ya kitaifa iliyohusisha zaidi ya nchi 50.

Je, Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu Mifumo ya Chakula unasaidiaje maandalizi na ushiriki wako katika ?

Katika zoezi la Umoja wa Mataifa la Thamini ya Mifumo ya Chakula, kila eneo la dunia litawasilisha nafasi yake. Msimamo wa Afrika utahusu masuala matatu muhimu.

La kwanza ni kufadhili mageuzi ya mifumo ya chakula. Inapaswa kuwa kipaumbele kwa washirika wetu kwamba uwezo wetu wa kutafuta rasilimali za ndani haudunishwi.

La pili ni tabianchi, ambayo itahitaji kuchunguzwa kwa namna ya kweli kabisa. Licha ya ahadi zilizotolewa katika COPS mbalimbali, ahadi hizo hazijatekelezwa. Ikiwa ahadi hizi haziwezi kuheshimwa, lazima tuchunguze mbinu mbadala za ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi.

La tatu ni kuhusu wakulima wetu wadogo. Wakulima ni sehemu ya sekta binafsi tunayoizungumzia. Sekta binafsi siyo kilimo biashara pekee; pia inajumuisha wakulima wadogo wadogo ambao wana uwezo na maarifa ya kubadilisha mifumo yetu ya chakula. Wanahitaji kufadhiliwa, kama inavyofanyika Marekani na Ulaya.

Katika zoezi la Tathmini, kitakachochunguzwa pia ni hatua tuliyopiga na kufikia katika kutekeleza mahitimisho ya Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula wa 2021 na mafunzo ambayo kanda zinawezafauidika nayo.

Huku makadirio ya idadi ya watu barani Afrika ikifikia takriban bilioni 2.5 ifikapo mwaka 2050, pamoja na changamoto iliyopo ya Waafrika zaidi ya milioni 250 wenye utapiamlo, je, kuna hali ya wasiwasi mkubwa miongoni mwa watunga sera na washikadau?

Swali hili ni muhimu sana kwa sababu idadi ya watu barani Afrika inatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo 2050. Wasiwasi mkubwa zaidi ni changamoto ya kuwalisha zaidi ya watu bilioni 1 zaidi. Kushindwa kushughulikia suala hili kwa uwezo na suluhisho zinazohitajika sio tu kwamba kutaathiri mifumo yetu ya utawala iliyopo bali pia kutakuwa na ongezeko la udhaifu wa kijamii.

Kwa kuzingatia hali yetu ya idadi ya watu, hatari ya kukumbana na majanga mengi ya kisiasa inakuwa wazi.

Dharura ni muhimu katika kutambua mtazamo kabambe na kuharakisha utekelezaji wa suluhisho, hasa ikizingatiwa kuwa sehemu kubwa ya makadirio ya ongezeko la watu tayari ipo.

Kuongeza kwa kasi hii lazima kufikiwe kupitia sera zinazofaa na maamuzi ya kisiasa.