爆料公社

Siku16 za Uanaharakati dhidi ya Dhuluma za Kijinsia

Get monthly
e-newsletter

Siku16 za Uanaharakati dhidi ya Dhuluma za Kijinsia

Kampeni inaanza tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba chini ya Mada: “Orange the World: End Violence against Women Now!”
Afrika Upya: 
24 Novemba 2021
 Jijini Dar es Salaam, Tanzania, wasichana wa shule huandaa maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsi
UN Women Tanzania/Deepika Nath
Jijini Dar es Salaam, Tanzania, wasichana wa shule huandaa maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku 16 za Unaharakati dhidi ya Dhuluma za Kijinsia kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba 2021, chini ya mada ya kimataifa iliyotungwa na kampeni ya UNiTE ya Katibu Mkuu wa UM: “!”

Mmoja kati ya wanawake watatu amewahi kudhulumiwa maishani mwake, kimataifa.? Katika nyakati za hatari, idadi hiyo inaongezeka, kama ilivyoshuhudiwa wakati wa janga la COVID-19 na hali ya maajuzi ya hatari, mizozo ma majanga ya tabianchi.?

Ripoti mpya kutoka UN Women, iliyozingatia data kutoka kwa mataifa 13 tangu kuzuka kwa janga hilo, inaonyesha kwamba wanawake 2 kati ya 3 waliripoti kwamba wao wenyewe au mwanamke wanayemfahamu alishuhudia aina fulani ya dhuluma na wamo katika hatari ya kukabiliwa na ukosefu wa chakula. Ni 1 tu kati ya wanawake 10 waliosema kwamba wahasiriwa wangetafuta msaada wa askari.

Kuwaamini wahasiriwa

Ingawaje zimeenea, dhuluma za kijinsia sio jambo lisiloepukika. Zinaweza na ni lazima zizuiliwe. Kuzikomesha dhuluma hizi kunaanza kwa kuwaamini wahasiriwa, kuchukua mielekeo kamilifu na jumuishi ambayo inakabiliana na vyanzo vyake, kubadilisha mienendo hasi ya kijamii, na kuwawezesha wanawake na wasichana.

Tunaweza kuangamiza dhuluma za kijinsia kukiwa na huduma msingi zinazompendelea mwathriwa za polisi, haki, afya, na sekta za kijamii, na ufadhili wa kutosha wa ajenda za haki za wanawake.

Ukumbi wa??uliokamilika jijini Paris mwezi wa Julai uliweka kasi ya hatua muhimu na uwekezaji wa kuendeleza usawa wa kijinsia. ?

Hazina ya UN ya Kuangamiza Dhuluma dhidi ya wanawake, njia ya pekee ya kimataifa ya kutoa ruzuku inayolenga kuangamiza na kuzuia aina zote za dhuluma dhidi ya wanawake, imetangaza njia maalumu ya kuchanga fedha,?, ikiadhimisha miaka 25 ya kutoa ruzuku ya kusaidia mashirika ya wanawake ulimwenguni.