±¬ÁϹ«Éç

Kongamano la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa

Get monthly
e-newsletter

Kongamano la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mkutano na Waandishi wa Habari na Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, kufuatia Mkutano wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
Africa Renewal
Afrika Upya: 
1 December 2021
 António Guterres
UN Photos
Katibu Mkuu wa UN António Guterres

Ninamshukuru Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika - rafiki yangu mpendwa Moussa Faki Mahamat.ÌýÌý

Tumehitimisha Kongamano la tano la Mwaka kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.Ìý ÌýÌý

Ushirikiano kati ya mashirika yetu una nguvu zaidi kuliko hapo awali.ÌýÌý

Na leo, tulipima ukuaji wetu na hatua zetu zinazofuata.ÌýÌý

Hatua hizi zinajumuisha kazi yetu ya pamoja ya kuendeleza amani na usalama barani Afrika; ushirikiano wa maendeleo; hatua za kibinadamu, uchaguzi, kubadilishana mamlaka kwa amani; naÌýMfumo mpya wa Pamoja wa Haki za Kibinadamu.Ìý

Tuliangazia masuala muhimu ya kufufua uchumi wa Afrika.ÌýÌý

Kwanza,Ìýkupiga hatua kuhusu chanjo - huku kukiwa na asilimia sita pekee ya wakazi wa Afrika waliopata chanjo kamili na aina mpya za COVID zinazotishia maisha na matarajio ya kupona.Ìý Ìý

Tumeona viwango vya chini vya chanjo - pamoja na ufikiaji usio na usawa wa chanjo – mambo yanayochangia kuenea kwa aina mpya za COVID.Ìý

Tunahitaji ushirikiano wa kweli kuhusu chanjo — sasa.ÌýÌý

Nilitoa wito kuwe na mpango wa kimataifa wa chanjo unaohusisha nchi zote zinazotengeza - auÌýzinazowezaÌýkutengeneza chanjo, zikiwemo nchi kadhaa barani Afrika.ÌýÌý

Kwa kukosekana kwa mpango kama huo, ninaunga mkono kikamilifu mkakati wa Shirika la Afya DunianiÌýwa kupata chanjo kwa asilimia 70 ya watu, katika nchi zote, katika miezi sita ya kwanza ya 2022.Ìý

Na tunahitaji kuendelea kuitisha usaidizi na ufadhili kwa ajili ya utengenezaji endelevu wa chanjo barani Afrika.ÌýÌý

Watu wa AfrikaÌýhawezi kulaumiwa kwa kiwango cha chini cha chanjo zinazopatikana kwao.ÌýÌý

Wala hawapaswi kuadhibiwa kwa pamoja kwa kutambua na kusambaza habari muhimu za kisayansi na afya na ulimwengu.Ìý

Kwa virusi ambavyo havina mpaka, vizuizi vya kusafiri vinavyotenga nchi au eneo fulani ni adhabu kali na utovu wa haki - haziwezi kufanya kazi.ÌýÌý

Badala yake, ninatoa wito kwa serikali zote kuzingatia upimaji wa mara kwa mara kwa wasafiri, pamoja na hatua zingine zinazofaa kwa kweli.ÌýÌý

Hii ndiyo njia ya pekee ya kupunguza hatari ya maambukizi huku ikiruhusu usafiri na ushirikiano wa kiuchumi.ÌýÌý

Pili, ulimwengu unahitaji kushughulikiaÌýmkondo wa ukosefu wa maadili na ukosefu wa usawa katika kufufua uchumi.Ìý

Nchi zilizostawi zinawekeza asilimia 28 ya Pato lao la Taifa katika kurejesha mapato, nchi zenye mapato ya kati zinawekeza asilimia 6.5, na nchi zilizoendelea kidogo zinawekeza asilimia 1.8 tu ya hela kidogo sana.ÌýÌý

Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Shirika la Fedha la Kimataifa linakadiria kwamba ukuaji wa uchumi kwa kila mwananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo utakuwa chini ya asilimia 75 kuliko mataifa mengine duniani.ÌýÌý

Hili halikubaliki kamwe. Afrika ilikuwa inaendelea vizuri sana kabla ya janga hili. Kwa miaka kumi Afrika ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wa dunia na sasa Afrika italazimika kulegea kwa sababu ya ukosefu wa mshikamano wa kimataifa.Ìý

Ni ukweli kwamba nchi zilizo katika hali ngumu zinazama kwenye madeni.ÌýÌý

Na wanategemea ugavi upya wa Haki za Mfuko Maalumu wa Fedha ambazo hazijatumika.Ìý Ìý

Lakini tunahitaji kujitolea kwa kiasi kikubwa kufanya hivyo, kwa sababu - kama unavyojua -Ìý zinasambazwa kwa nchi tajiri zaidi duniani.Ìý

Mkakati wa Kusimamisha Ulipaji wa Madeni wa G20 lazima uendelezwe hadi mwaka ujao.ÌýÌý

Nchi zote zinazoendelea - ikijumuisha nchi za mapato ya kati - zinahitaji msaada bora wa madeni.Ìý

Kisha, hatua za mabadiliko ya hali ya hewa.Ìý Ìý

Lengo la kupunguza ongezeko la joto hadi digrii 1.5 limelemaa, kama unavyojua.Ìý

Na wale wanaochangia kiwango cha chini cha joto hilo wanapata athari kali zaidi.ÌýÌý

Nchi tajiri zaidi zinahitaji kuimarisha kwa kiasi kikubwa msaada wake kwa nchi zinazoendelea - kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo na kugeukia uchumi wa kijani.ÌýÌý

Na hatimaye, ufufuo unamaanisha kujenga amani ya kudumu katika eneo linalokumbwa na mizozo na misukosuko ya kisiasa.Ìý Ìý

HiiÌýinategemea kuwekeza katikaÌýshughuli za usaidizi wa amani zinazoongozwa na Umoja wa AfrikaÌý— na nitaendelea kusukuma ili kuhakikisha wana idhinoi ya Baraza la Usalama chini ya Sura ya VII ya Mkataba na ufadhili.Ìý

Katika miezi ya hivi karibuni tumeshuhudiwa kuibuka tena kwa mapinduzi ya kijeshi.Ìý Ìý

Tunashuhudia ugaidi na itikadi kali kali zikinyemelea mamilioni ya watu kote Sahel na mapigano mapya nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.ÌýÌý

NaÌýmzozo nchini Misri unaendelea bila kukoma.Ìý

Ninatoa wito tena wa kukomesha mara moja uhasama na ufikiaji usiokwazwa wa kibinadamu.ÌýÌý

Hakuna uhalali wa kulenga makundi ya kikabila na kukamatwa kiholela - wala kuwaweka kizuizini wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.ÌýÌý

Kazi hii yote inahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika - na hiyo ndiyo ajenda ya mkutano wa leo.ÌýÌý

Kwa mara nyingine tena, napenda kumshukuru Mwenyekiti Faki na natazamia ushirikiano wa kina zaidi katika siku za usoni.ÌýÌý

Asante.

Ìý

Ìý

Mada: