Ϲ

Umoja wa Afrika (AU) ushinikize usawa katika upatikanaji wa chanjo za COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Umoja wa Afrika (AU) ushinikize usawa katika upatikanaji wa chanjo za COVID-19

Upatikanaji unahitaji mshikamano wa kimataifa, teknolojia ya pamoja na kuondoa masharti ya Haki Miliki.
Carine Kaneza Nantulya
Afrika Upya: 
6 January 2021
Wafanyakazi wa afya wakifanya kazi katika Maabara ya Upimaji ya Hospitali Kuu ya Mpilo19 huko...
KB Mpofu / ILO
Wafanyakazi wa afya wakifanya kazi katika Maabara ya Upimaji ya Hospitali Kuu ya Mpilo19 huko Harare, Zimbabwe.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti hii iko kwa Kiingereza.

Julia Mwangaza* ni mtaalamu wa afya mwenye umri wa miaka 41 anayehudumu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi nchini Tanzania. Nilipozungumza naye hivi majuzi, alieleza hofu yake kwamba, kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya COVID-19 katika eneo hilo, watoa huduma za afya wataelemewa hivi karibuni na kushindwa kuwatunza wagonjwa.

Bi. Mwangaza pia alikuwa na wasiwasi na kutokumalizika kwa COVID-19 na athari yake kwa jamii.

“Nina wasiwasi kama sisi watu maskini tutakuja kupatiwa chanjo,” alisema. "Labda kama wanaogopa tutawaambukiza, nchi za Magharibi haziwezi kuwa na ukarimu kiasi hicho."

Wakati nchi kama vile Marekani na Uingereza zimeshaagiza idadi kubwa ya dozi za chanjo, waafrika wengi wanajiuliza kama kutakuwa na usawa na haki katika uzalishaji na usambazaji.

"Ikiwa nchi tajiri zitaendelea kuongeza mgao wao wa mpango huu, itachukua muda mrefu sana kwa mwafrika wa kawaida kupata chanjo," anasema Daniel Ncube*, daktari kutoka Zimbabwe.

Bi. Mwangaza, Dkt. Ncube na wahudumu wengine wa afya kutoka Afrika na wataalamu ambao nimewahoji katika kipindi cha wiki chache zilizopita wana kila sababu ya kuwa na wasiwasi.

Mwezi Oktoba, shirika la Human Rights Watch lilichapisha inayoangazia suala la kutatiza kwamba serikali za nchi tajiri, zilizo na rasilimali kuagiza mapema mamilioni ya dozi za chanjo za COVID-19 ambazo kwa sasa, hazipatikani kwa wingi. Hii inamaanisha kwamba nchi zenye uchumi wa chini na wa kati zitalazimika kusubiria chochote kitakachobakia.

Carine Kaneza Nantulya
Carine Kaneza Nantulya, mkurugenzi wa utetezi wa Afrika katika Human Rights Watch.

Mnamo Septemba 2020, shirika la kimataifa la Oxfam kwamba nchi zenye mapato ya juu tayari zimeagiza asilimia 51 ya dozi kutoka kwa asasi mbalimbali zinazoongoza kutoa chanjo, ingawa nchi hizo ziliwakilisha asilimia 13 tu ya idadi ya watu duniani.

Global Justice Now mnamo Novemba 2020 kwamba zaidi ya asilimia 80 ya dozi za chanjo za Pfizer na BioNTech tayari zimenunuliwa na nchi chache tu – zote zikiwa ni nchi zilizoendelea zilizo nje ya Afrika.

Tarehe 7 Novemba 2020, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, alifanya mkutano na viongozi wengine wa Afrika ili kuweka mikakati kuhusu namna ya kupata na kufadhili chanjo za COVID-19 barani Afrika, ambayo inakadiriwa kugharimu dola bilioni 12.

Dkt. John Nkengasong, mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC) alikadiria kwamba ingechukua bilioni 1.3 barani Afrika, kwa dozi mbili kwa kila mtu.

Japokuwa chanjo zimeanza kutolewa nchini Marekani na Uingereza, huenda zisifike katika nchi za Afrika hadi katikati ya mwaka 2021, Dkt. Nkengasong alionya.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kwamba huenda ikafika kuweza kutoa chanjo dhidi ya COVID-19 dunia nzima.

Army Spc. Angel Laureano holds a vial of the COVID-19 vaccine. Photo: Lisa Ferdinando
Chombo cha chanjo ya COVID-19 Picha: Lisa Ferdinando

Serikali za Afrika na AU zinaweza kusadia mipango mitatu mikuu ili kuhakikisha kwamba bara hili haliachwi nyuma katika vita vya kukomesha janga hili:

Mpango wa kwanza ni Kituo cha COVAX, mpango wa kimataifa unaoleta pamoja serikali na watengenezaji wa chanjo ili kuhakikisha kwamba chanjo za COVID-19 zinawafikia wale wanaozihitaji zaidi. Mpango huu una uwezo wa kunufaisha nchi za Afrika iwapo utafaulu kupata chanjo za kutosha kusambaza kwa bei nafuu ili kuzipunguzia madeni.

Lakini hata kwa msaada huu, bara hili haliwezi kupata dozi za kutosha kutoa chanjo kwa asilimia 60 ya watu. Hii ndiyo sababu mipango mingine miwili ya kimataifa ni muhimu katika kushughulikia upungufu wa chanjo na kuhakikisha usawa katika ufikiaji wa chanjo kwa wote unatimizwa.

Mnamo Mei 2020, serikali ya Costa Rica iliongoza kuunda Kitovu cha Ufikiaji wa Teknolojia cha COVID-19 (C-TAP), kitovu cha pamoja cha haki za teknolojia, takwimu na ujuzi ambao kila mtu duniani kote angeutumia kutengeneza bidhaa zozote za matibabu zinazohitajika ili kupambana na COVID-19, ikiwemo chanjo.

Kufikia Desemba 2020, nchi sita pekee barani Afrika – Misri, Msumbiji, Afrika Kusini, Sudan, Tunisia na Zimbabwe – ndizo zilikuwa zimeidhinisha Mwito wa Kuchukua Hatua wa Umoja wa C-TAP, ambao ni mpango wa pili.

kanuni , ni mpango wa tatu uliopendekezwa mnamo mwezi Oktoba 2020 na India na Afrika Kusini. Ilipendekezwa kuondoa baadhi ya kanuni za Mkataba kuhusu Vipengele Vinavyohusiana na Biashara ya Haki Miliki (TRIPS), mkataba wa kisheria wa kimataifa baina ya wanachama wote wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO).

Uondoaji wa kanuni hizi unaopendekezwa unaruhusu nchi zote duniani kushirikiana katika kupambana na COVID-19, ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kusambaza chanjo, bila kuzuiwa na ugumu wa sheria na vikwazo vinavyotawala haki miliki. Nchi kama vile Kenya, Eswatini na Msumbiji zimejiunga ili kuunga mkono pendekezo hilo.

Dkt. Solomon Ayele Dersso, mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Afrika (ACHPR) hivi majuzi Umoja wa Afrika uongoze mpango huu kwa niaba ya Afrika. Wataalamu wengine wa mashirika ya kimataifa pia pendekezo hili la kuondoa kanuni.

Miito hii tofauti inadhihirisha kwamba serikali za Afrika na AU ni lazima zishughulike kwa haraka ili kuhakikisha wananchi wao wanaweza kuzifikia chanjo za COVID-19.

Nchi nyingine 48 za Afrika zilizosalia zinapaswa kujiunga na Misri, Msumbiji, Afrika Kusini, Sudan, Tunisia na Zimbabwe ili kuidhinisha na kutekeleza mpango wa WHO wa C-TAP unaohitaji kuwepo kwa leseni huru ya haki miliki isiyobagua ili kunufaika zaidi na utafiti wa kisayansi.

Kadhalika, mataifa mengine wanachama wa AU yanapaswa kuunga mkono pendekezo la India na Afrika Kusini katika WTO kutumia vipengele TRIPS vinavyoweza kubadilika katika ngazi ya nchi. AU inaweza kuitisha mkutano wa marais wa nchi za AU na Serikali kwa lengo la kuunga mkono pendekezo la uondoajiwa kanuni za TRIPS ili kutoa ujumbe thabiti wa ushirikiano huo.

Mataifa wanachama wa AU yanapaswa kushinikiza kuwepo kwa masharti thabiti kuhusu ufadhili wote wa utafiti, ukuzaji, utengenezaji na usambazaji wa chanjo ya COVID-19 unaohitaji uhamishaji wa teknolojia. Haya yatahakikisha ushirikiano wa haki miliki, takwimu na ujuzi mwingine ili kuwezesha utengenezaji chanjo kwa wingi kwa asasi zilizofanikiwa kutengeneza chanjo hio.

AU na Mataifa wanachama yanaweza kuchukua hatua hizi chache thabiti ili kuhakikisha usawa, uwazi na haki katika utengenezaji na usambazaji wa chanjo za COVID-19.

Maisha pamoja na afya ya Bi. Mwangaza, Dkt. Ncube na mamilioni ya Waafrika wengine huenda yakaitegemea.


*Si jina lake halisi

Bi. Nantulya ni mkurugenzi wa utetezi Barani Afrika katika shirika la Human Rights Watch.

Carine Kaneza Nantulya
More from this author