±¬ÁϹ«Éç

AfCFTA: Jinsi Hakimiliki inavyoweza kusaidia kutengeneza ajira

Get monthly
e-newsletter

AfCFTA: Jinsi Hakimiliki inavyoweza kusaidia kutengeneza ajira

Soko moja ni njia yenye uwezo wa kuongeza kasi ya ukuaji wa Biashara Ndogondogo ambazo huleta asilimia 80 ya ajira barani Afrika.
Afrika Upya: 
5 January 2021
Mfanyabiashara katika duka lake la vifaa vya elektroniki kwenye soko huko Treichville, Abidjan...
Jennifer A. Patterson/ILO
Mfanyabiashara katika duka lake la vifaa vya elektroniki kwenye soko huko Treichville, Abidjan, wakati wa mgogoro wa COVID-19.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti hii iko kwa Kiingereza.

Mkataba unaoanzisha Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) una matazamio makubwa. ÌýMkataba huu unayaleta pamoja mataifa 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, na utaunda eneo kubwa zaidi huru la biashara duniani kwa idadi ya nchi zinazoshiriki.

Pia utaanzisha soko moja ambapo bidhaa, huduma na watu wanaweza kusafiri kwa ufanisi, wakipanua vyema biashara ya ndani ya bara la Afrika, kuongeza ushindani na kusaidia mabadiliko ya kiuchumi.

Mkataba huu unashugulikia biashara ya bidhaa na huduma, uwekezaji, hakimiliki na sera ya ushindani. Mazungumzo ya Awamu ya Pili ya mkataba yana fursa nyingi, haswa katika eneo la hakimiliki.

Hakimiliki kwa asili ni za eneo ama nchi husika, kwa maana hiyo sheria za kitaifa ndio Ìýzinasimamia Ìýupatikanaji, utunzaji na utekelezaji Ìýwake.

Sheria za Hakimiliki zinaweza kutumiwa kama chombo cha kuchochea ubunifu na kuwezesha maendeleo kupitia kufichua na kuhamisha maarifa na ujuzi.

Kifungu cha 4 cha Mkataba wa AfCFTA kinaelezea ushirikiano wa nchi wanachama katika Ìýuwekezaji, hakimiliki na sera ya ushindani. Kwa hivyo, mazungumzo katika Awamu ya II yanapaswa kuangazia kupatikana kwa soko moja barani Afrika.

Soko moja linasifiwa kama kichocheo cha kukuza ukuaji wa Biashara Ndogondogo. Kulingana na Jukwaa la Uchumi Duniani, Biashara Ndogondogo zinatoa zaidi ya asilimia 80 ya ajira za Afrika (katika soko la watu wapatao bilioni 1.2) na kuchangia hadi asilimia 50 ya Pato la Taifa (GDP). Kwa hivyo, Taratibu za Hakimiliki zinatarajiwa kuwezesha ukuaji wa Biashara Ndogondogo kwa njia nyingi.

Jinsi Taratibu za Hakimiliki zinavyoweza kuchangia ukuaji wa Biashara Ndogondogo

Kwanza, taratibu za Hakimiliki zinapaswa kuzingatia kuondoa upendeleo wa nchi za AfCFTA ikilinganishwa na nchi zilizo nje ya Afrika. Tofauti hii inatokana na ushiriki wa nchi tofauti katika mikataba tofauti ya Hakimiliki za kimataifa na mataifa mawili. Kwa mfano, nchi zingine sio wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kwa hivyo hazifaidiki kwa kanuni kadhaa za kimataifa ya Hakimiliki kama upendeleo wa kitaifa na taifa linalopendelewa zaidi.

[Katika biashara ya kimataifa, kifungu cha taifa linalopendelewa zaidi (MFN) kinahitaji Ìýnchi Ìýkutoa maridhiano, upendeleo au kinga katika makubaliano ya biashara Ìýbaina ya nchi wanachama wa Shirika la Biashara Duniani. Ingawa jina lake linaashiria upendeleo kwa taifa lingine ila Ìýinaashiria kutendewa kwa Ìýsawa kwa nchi zote. Kwa upande mwingine, kifungu cha kutendewa kitaifa kinakataza ubaguzi kati ya raia wa Mwanachama na raia wa Wanachama wengine].

Pili, Taratibu za Hakimiliki zinapaswa kujiimarisha kwa Ìýkupitia mifumo iliyopo ya Hakimili ya kikanda, kama vile ARIPO na OAPI ili kurahisisha sera za Hakimiliki za bara. [Afrika ina mifumo miwili ya hatimiliki ya kikanda, OAPI (Organisation Africaine de la Propriété Intellectuelle au Shirika la Hakimiliki ya Afrika) na ARIPO (Shirika la Kikanda la Hakimiliki la Afrika). Ìý

Ingawa nchi zenye uchumi mkubwa za Afrika kama vile Afrika Kusini, Nigeria na Misri sio sehemu ya mifumo ya kikanda, mifumo ya OAPI na ARIPO hutoa njia nafuu, rahisi na bora ya kupanua ulinzi wa Hakimiliki kwa jumla ya nchi 35 za Afrika zenye Pato la Taifa lililojumuishwa la dola bilioni 420].Ìý Taasisi hizi zinapaswa kupewa msaada kwa utekelezaji mzuri wa sera.

Mwisho, taratibu za Hakimiliki zinapaswa kuzingatia kufungua soko la bara la Afrika. Katika masuala ya Hakimiliki, hii inaweza kufikiwa kupitia sheria na sera za Mataifa wanachama kuhusu kutumia haki.

Kutumia haki (pia inajulikana kama kanuni ya kwanza ya uuzaji) inasema kwamba mahali ambapo mmiliki wa hakimiliki anapoweka bidhaa au kazi iliyolindwa katika soko, hawawezi tena kuzuia uuzaji wake. Soko katika hali hii kawaida huwa na mipaka ya kijiografia.

Hivi sasa, nchi zina sera tofauti kuhusu matumizi ya haki. Kenya, kwa mfano, inatumia haki za kimataifa, wakati Rwanda inatumia haki za kitaifa. Sheria na sera zinapaswa kusawazishwa ili kuleta matumizi ya kikanda, na kufanya eneo lote la Afrika litazamwe kama soko moja kulingana na malengo ya AfCFTA.
Ìý
Matumizi yanamaanisha matumizi ya haki katika mada ya Hakimiliki kama matokeo ya uhamishaji halali wa mada katika kifungu halisi ambacho kinajumuisha au kubeba mali ya Hakimiliki husika.Ìý
Ìý
Matumizi hutokea wakati mmiliki wa hakimiliki anahamisha umiliki wa kipengele fulani cha haki hiyo, au bidhaa ya watumiaji inayouzwa chini ya haki fulani ya Hakimiliki. Upeo wa kijiografia unamaanisha mipaka ya kijiografia, ambayo uuzaji lazima ufanyikie, au kifaa hicho kinapaswa kutengenezwa, ili kuchochea matumizi.
Ìý
Chini ya matumizi ya kitaifa, hakimiliki kwa kifaa fulani imetumika tu ikiwa kinauzwa au kimetengenezwa ndani ya nchi ambayo sheria za Hakimiliki za mmiliki zimeombwa. Kwa matumizi ya kimataifa, eneo la uuzaji au utengenezaji halina umuhimu, na uhamishaji wowote wa umiliki ulioidhinishwa husababisha matumizi].

Mbali na vifungu vya jumla vya ushirikiano na nchi wanachama, Taratibu za Hakimiliki zinapaswa pia kuzingatia mifumo ya Hakimiliki ambayo haitumiwi vya kutosha barani Afrika, ikijumuisha viashiria vya kijiografia, ulinzi wa anuwai ya mimea na ulinzi wa rasilimali za maumbile, maarifa ya jadi na misemo ya kitamaduni.

Viashiria vya Kijiografia

Viashiria vya kijiografia ni ishara inayotumiwa kwenye bidhaa zilizo na asili maalum ya kijiografia na zina sifa zinazotokana na mahali pa asili. Barani Afrika, aina hii ya ulinzi ni muhimu kwani bidhaa za kilimo za Afrika kawaida zina sifa ambazo zinatokana na mahali pao Ìýpa uzalishaji na zinaathiriwa na masuala maalum za kijiografia ya eneo husika.

Kifungu cha 22.2 cha Mkataba wa Shirika linaloshugulikia masuala ya Biashara Duniani(WTO) Ìýkuhusu Vipengele Vinavyohusiana na Biashara vya Hakimiliki kinaruhusu nchi kuamua ni aina gani ya ulinzi utakaofaa kwa viashiria vya kijiografia. Barani Afrika, nchi zingine, kama vile ÌýKenya na Afrika Kusini, zinalinda viashiria vya kijiografia chini ya sheria ya Alama ya Kibiashara huku nchi zingine, kama vile Morocco na Uganda, zina sheria Ìýtofauti.

Mwaka wa 2017, Umoja wa Afrika uliridhia Mkakati wa Kidunia wa Viashiria vya Kijiografia. Mkakati huu unatambua umuhimu wa viashiria vya kijiografia kama nyenzo ya matumizi katika maendeleo endelevu vijijini na usalama wa chakula.

Kwa hivyo, jamii zitaweza kuimarisha sifa za kipekee za kiuchumi za bidhaa za kilimo kulingana na maeneo yao ya uzalishaji. Matumizi ya faida zinazohusiana na viashiria vya kijiografia na jamii yanatarajiwa kusababisha maendeleo ya uchumi haswa kwa wanawake na vijana.

Kulinda maarifa ya Kitamaduni ya Asili

Afrika ina utajiri na maarifa anuwai—tamaduni ambazo ni za kipekee kwa watu binafsi na jamii barani humo. Maarifa ya jadi ya jamii za wenyeji yanapaswa kuzingatiwa katika Taratibu za hakimiliki kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Taratibu zinapaswa kutoa mahitaji ya kiwango cha ulinzi wa maarifa ya jadi, rasilimali za kimaumbile na misemo ya kitamaduni. Maarifa ya jadi yaliyopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine yamesababisha ugunduzi wa dawa na suluhisho zingine za kibunifu. Kwa kuwa na miongozo sahihi juu ya ulinzi wa maarifa ya jadi na misemo ya kitamaduni, jamii zitaweza kufaidika kiuchumi kupitia uhamishaji wa maarifa haya.

Ulinzi unaotolewa lazima uwe wa ni wa kutetea. Hii itawezesha jamii kukuza maarifa yao ya jadi, kudhibiti matumizi yake na kunufaika kwa matumizi yake ya kibiashara.

Kuendelea mbele

Malengo ya Mkataba wa AfCFTA yanaweza kutekelezwa iwapo Taratibu za Hakimiliki zitazingatia uunganishaji wa sera na sheria kwa kuweka viwango na kushughulikia vyema mambo ya hakimiliki katika biashara barani Afrika na ambayo ulinzi wao unaweza kufungua njia za kuingiza mapato nchini.

Mfumo madhubuti wa hakimiliki barani kote utarahisisha ukuaji wa Biashara Ndogondogo na utasababisha ongezeko la kutengeneza ajira haswa kwa wanawake na vijana.


Bi. Mbatia na Bi. Vilita ni mawakili wa Hakimiliki katika shirika la Mawakili la CFL lililoko jijini Nairobi na Kigali. lorna@cfllegal.comÌý

More from this author