±¬ÁĎą«Éç

Kugeuza taka kuwa utajiri

Get monthly
e-newsletter

Kugeuza taka kuwa utajiri

Katika shule moja ya Uganda, wanafunzi wapata pesa kutokana na uhifadhi
Melissa Kyeyune
Afrika Upya: 
6 August 2019
A student holding an SDG badge (top).
Photo: Solomon Musisi
Students holding vegetables from the school garden.

Namugongo ni eneo la katikati mwa Uganda lililostawi kijanikibichi na lenye jamii ya msitu ambako miti mirefu ni hifadhi ya ndege wa rangi maridadi na tumbili wenye kelele nyingi. Jamii hiyo ina historia ya tanzia:Ěý tarehe 3 Juni 1886, raia wa Uganda waliobadili dini waliuawa kwa kufuatia amri ya Mfalme Mwanga II wa ufalme wa Baganda. Alifanya hivi akijaribu kuzuia athari za utawala wa kikoloni ambao ulihusishwa na Wakristo.

Wafiadini hao walikwezwa katika utakatifu na Papa Mtakatifu Paul VI mwaka wa 1964.

Siku hizi Waganda huwaona wahanga hao kama mashahidi wa kidini. Wanaadhimisha kila tarehe 3 Juni kama Siku ya Mashahidi wa Kidini. Huwa na sherehe za wiki nzima ambazo huvutia maelfu ya wageni kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.Ěý ĚýĚý

Katika juma hilo, wanaosherehekea hutupa tani nyingi za taka, zikijumlisha chupa za plastiki, vyakula na majitaka, aghalabu wakizirusha katika mitaro iliyo wazi, ambako zinaweza kusafirishwa kwa mvua kubwa hadi katika majengo ya Shule ya Mtakatifu Kizito, pembeni mwa kijiji.

Kutoka taka hadi utajiri

Lakini wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Kizito wamejitokeza na mbinu za kukusanya taka hizo na kuzigeuza kuwa utajiri. Wanatumia mchangatope wanaoukusanya kuunda na kuhifadhi mapito ya shule yaliyotandazwa, na kuunda vinyago na bidhaa za kiufundi kutokana na mirija ya plastiki na chupa, ambavyo wanauza baadaye. Wanafunzi hao pia wanageuza taka zinazotokana na mimea au vyakula kutengeneza mbolea kwa matumizi ya mashamba ya shule, ambako wanajifunza kukuza mayoga, vitunguu na kabeji, na wanatumia matofali ya kuchomwa kutoka kwa taka zinazooza kama makaa kupika chakula.

A student holding an SDG badge. Photo: Solomon Musisi
A student holding an SDG badge. Photo: Solomon Musisi

Unapotembela shule hiyo unagundua juhudi nyingi za uundaji upya unaofanywa na wanafunzi. Vitanda vitatu vikubwa vya fremu za chuma vimeundwa upya na wanafunzi kuwa chombo sahili cha kutenga taka kilichowekwa katikati mwa uwanja wa shule. Hapa wanafunzi wanatenga taka tofauti: karatasi, plastiki na vitu vyenye uwezo wa kuoza.

“Tunapata mirija michafu, kisha tunailainisha. Baadaye tunaishona kuwa vikapu, begi za mikononi, pochi za kubebea pesa, begi za vipakatalishi, mikeka ya milangoni na mazulia. Tunawauzia wazazi wetu na wageni bidhaa hizo,” anasema Patricia Nakibuule, mmoja wa wanafunzi watengenezao bidhaa hizo kwa mikono.

“Nina jukumu la kuhakikisha kwamba wanafunzi wenzangu, wote 800 wamepata chamcha,” anasema akitabasamu. “Tunatumia matofali ya kuchoma yalioundwa kwa taka zinazooza kama makaa kwa kuwa hili linachangia uundaji upya na kupunguza ukataji miti.” Shule haihitaji kuni, kwa hivyo haina haja ya kukata miti msituni.

Mbali na kuunda upya vifaa kutokana na taka, Shule ya Mtakatifu Kizito inawapa wanafunzi ujuzi wa kuunda sabuni na mishumaa, kutunza wanyama, kuyafanya mazingira yapendeze na kuoka.

Wanafunzi wasimulia visa vyao

“Ninafuga ndege na kukuza nyanya nyumbani, kwa hivyo wazazi wangu hawatumii pesa nyingi kwa vyakula,” anasema Christine Nandujja, ambaye anaeleza kuwa anatumia mbinu za kilimo bora ajifunzazo shuleni anapokuwa nyumbani.Ěý

Joseph Kakande, kiranja wa michezo katika shule hiyo, anafurahia ukuzaji mboga kama afanyavyo mpira wa vikapu. “Nilijifundisha namna ya kukuza vitunguu na mayoga shuleni, kisha nikaanza kuzikuza nyumbani. Ulianza kama mradi mdogo, ila sasa ninakuza vya kutosha kuuza katika hoteli. Nilitumia faida yake kulipa nusu ya karo yangu muhula uliopita.”

Ili kuwapa mafundisho wanafunzi wa sasa, shule inawahusisha wanafunzi waliofuzu awali na wataalamu wengine wachanga katika miradi ya kubadili-taka-kuwa-kawi. Brian Galabuzi, Afisa Mtendaji wa WEYE Clean Energy Company, mradi wa kubadili-taka-kuwa-kawi, anawapa vijana mafundisho ya usimamizi wa taka na kawi safi na hutumia shule kama maabara kwa mipango yake inayoshinda tuzo mbalimbali.

Brian (WEYE Clean Energy) displays a  bag of briquettes. Photo: Solomon Musisi
Brian (WEYE Clean Energy) displays a bag of briquettes. Photo: Solomon Musisi

Aliambia Africa Renewal, “Nilipokuja shuleni kwa mara ya kwanza miaka michache iliyopita, nilikuwa mwanafunzi mchanga wa chuo kikuu na mawazo ya kichizi, ila wanafunzi waliyakumbatia. Walikuwa wametoka mashambani na kuona mawazo yangu kama fursa ya kuboresha ujuzi wao wenyewe. Nilinufaika sana na msaada wao.”

Leo Bwana Galabuzi asafiri duniani, akionyesha jinsi ya kugeuza taka kuwa kawi safi.

Rhoda Nassanga, mhandisi na mtaalamu wa uhifadhi wa maji, huwapa wanafunzi mafundisho kila mara. “Shabaha yangu ni kuwapa wanafunzi hawa maarifa wakiwa shuleni na kuwafundisha kuhusu malengo ya maendeleo endelevu,” anasema Bi. Nassanga. Ananufaika pia, kwa kuwa kuwapa wanafunzi afundisho kunamwezesha kutumia ujuzi wake wa uhandisi.

Athari chanya kwa jamiiĚý

Wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Kizito wamekuwa wakiwafundisha wakazi wa jamii ya Namugongo kuunda bidhaa za Sanaa na kiufundi kutoka kwa taka za plastiki, na kujipatia mapato.

Kwa sasa wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu kizito pamoja na jamii pana ya Namugongo wanafanya juhudi kutunza mazingira, kubuni biashara isiyodhuru mazingira, kusimamia miradi ya kimazingiraĚý na kutumia raslimali za asilia kwa njia endelevu.ĚýĚý

Frederick Kakembo, Mkurugenzi wa Shule ya Upili ya Mtakatifu Kizito, ambaye ana mafunzo ya awali katika Maendeleo ya Jamii, anaarifu “Ninaamini kuwa unastahili kutumia ulicho nacho kwanza kabla ya kutafuta kwingineko.”

Melissa Kyeyune
More from this author