Ϲ

Wakimbizi wa ndani DRC hatarini sababu ya COVID-19, vita na ukata -UNHCR

Get monthly
e-newsletter

Wakimbizi wa ndani DRC hatarini sababu ya COVID-19, vita na ukata -UNHCR

UN News
12 June 2020
By: 
Mkimbizi wa Sudan Kusini na mtoto katika makazi ya Bele katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
UNHCR/Jean-Jacques Soha
Mkimbizi wa Sudan Kusini na mtoto katika makazi ya Bele katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakati janga la virusi vya corona au na vita vikiendelea kushika kasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari kubwa ya Maisha yao kutokana na ukata wa kufadhili shughuli za misaada ya kibinadamu kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Akizungumza kwa njia ya mtandao na waandishi wa Habari mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa Babar Baloch amesema“pengo kubwa la ufadhili linatishia maelfu ya maisha ya watu DRC ambako machafuko na janga la COVID-19 vimeongeza madhila kwa hali ambayo tayari ilikuwa mbaya kwa mamilioni ya watu waliolazimika kukimbia makwao.”

Hadi kufikia Juni 7 mwaka huu DRC ilikuwa imethibitisha wagonjwa 4,105 wa COVID-19 ikiwa ni nchi ya pili kwa wagonjwa wengi Kusini mwa Afrika.

Wakati huohuo UNHCR inasema wimbi la machafuko limewafurusha maelfu n kwa maelfu ya watu Mashariki mwa nchi hiyo na limeonya kwamba bila hatua za haraka za kupata fedha , ukata utakuwa namadharamakubwa katika mipango ya kibinadamu ya kuokoa maisha ya shirika hilo.

“Shughuli zetu za kusaidia na kulinda wakimbizi na wakimbizi wa ndani zimefadhiliwa kwa asilimia 20 tu kati ya dola milioni 168 zinazohitajika. Pengo hili linakwamisha vibaya shughuli zetu za kufikisha msaada wa kibinadamu kwa mahitaji mbalimbali ya haraka na kuwaacha mamilioni ya watu bila chakula, maji, malazi, huduma za afya na usafi wakayi huu wa katikati ya janga la COVID-19 nchi nzima,”,ameongeza Baloch.

DRC ndiyo yenye idadi kubwa Zaidi ya wakimbizi wa ndani Afrika na ina asilimia 10 ya idadi ya wakimbizi wote wa ndani duniani.