±¬ÁϹ«Éç

Wakimbizi 7,500 wa DRC waingia Uganda; UNHCR

Get monthly
e-newsletter

Wakimbizi 7,500 wa DRC waingia Uganda; UNHCR

UN News
By: 
Wakimbizi waliotoroka vita nchini DRC wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa na kuhakikiwa kwenye kituo cha uandikishaji cha Oruchinga nchini Uganda. Picha na UNHCR/Michele Sibiloni
Picha na UNHCR/Michele Sibiloni. Wakimbizi waliotoroka vita nchini DRC wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa na kuhakikiwa kwenye kituo cha uandikishaji cha Oruchinga nchini Uganda
Picha na UNHCR/Michele Sibiloni. Wakimbizi waliotoroka vita nchini DRC wakiwa kwenye foleni wakisubiri kusajiliwa na kuhakikiwa kwenye kituo cha uandikishaji cha Oruchinga nchini Uganda

Watu zaidi ya 7,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wamekimbilia Uganda kusaka hifadhi kufuatia mashambulizi mapya katika jimbo la Ituri mahsariki mwa nchi hiyo.Ìý

Tangu kuzuka upya kwa mapigano ya kikabila mapema wiki hii, wakimbizi zaidi ya 400 wamesajiliwa kwenye kambi ya wakimbizi wa Kyangwali wilayani Kikuube.

Hao ni sehemu ya wakimbizi zaidi ya 7,500 ambao wamepokewa tangu mwanzo wa mwaka huu wakikimbia mapigano yaliochacha kwa misingi ya kikabila na pale vikosi vya jeshi laserikali ya DRC vinapopambana na vikundi vya katika maeneo ya Reso na Bulukwa.

Dunia Aslam Khani, Afisa wa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mtaifala kuhudumia wakimbizi (UNHCR) amesema wakimbizi hao wanavuka Ziwa Albert kwa boti hatarishi hadi kwenye Mwalo wa Sebagoro katika tarafa ndogo ya Kabwoya.

Ameongeza kuwa UNHCR na wadau wake wako tayri kuwapokea na kuwasafirisha hadi katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali haraka iwezekanavyo ili kupunguza msongamano kwenye mapokezi ya Sebagoro.

Hata hivyo,amesema ujio wao umebua upya chanagmoto katika utoaji wa huduma za mapokezi kwani asilimia kubwa yao ni wanawake na watoto.

Kutokana na hofu ya mambukizoya ebola sasa UNHCR na wadao wake likimemo shirika la la Afya DunianiÌý (WHO) na wizara ya afya ya serikali ya Uganda wameimarisha ufuatiliaji wa kiafya amabpo wakimbizi wote wanachekechwa.

Baadhi ya wakimbizi wanatoka katika maenneo mlimo ripotiwa mlipuko wa ebola.

Mozozo wa kikabila kati ya Walendu na Wagegere kuhusiana na umiliki wa ardhi umelazimisha maelfu kikimbia makwao tangu mwaka jana.