Ϲ

Tunajizatiti kurekebisha hali mji mkuu wa Kenya, Nairobi-Gavana Sonko

Get monthly
e-newsletter

Tunajizatiti kurekebisha hali mji mkuu wa Kenya, Nairobi-Gavana Sonko

UN News
By: 
Sehemu ya mji wa Nairobi ambako kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na Matatu, watu wanaweza kuathiriwa afya zao. Picha: Julius Mwelu/UN-Habitat
Picha: Julius Mwelu/UN-Habitat. Sehemu ya mji wa Nairobi ambako kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na Matatu, watu wanaweza kuathiriwa afya zao.
Picha: Julius Mwelu/UN-Habitat. Sehemu ya mji wa Nairobi ambako kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na Matatu, watu wanaweza kuathiriwa afya zao.

Nairobi tumezingatia masuala ya miji endelevu kwa ajili ya maendeleo na bado tunajizatiti kuhakikisha tunachukua hatua ili jiji letu liwe endelevu, amesema Gavana wa mji huo mkuu wa Kenya, Mike Sonko jijini New York, Marekani.

Akihojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhutubia mkutano wa wakuu wa miji na mameya wenye kauli mbiu: Kutoka masuala ya kimataifa hadi vipaumbele mashinani uliofanyika kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani Gavana Sonko amesema pamoja na hatua hizo bado Nairobi inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo uzoaji taka, lakini pia suala la usalama bado ni mtihani.

(Sauti ya Mike Sonko)

"Kulikuwa na shidashida kutokana na vijana kukosa kazi, wizi ulikuwa mwingi lakini naishukuru serikali kuu kupitia Rais Kenyatta tunafanya kazi vizuri na polisi na wakati tunapohitaji msaada wao tunawaita wale wa karibu. Tuna uhusiano mzuri na polisi wa Kenya na tunajaribu kwa kadri ya uwezo wetu. Pia tumejaribu kuwaajiri vijana kadhaa ingawaje sheria haituruhusu kumwajiri kila mtu, kwa sababu idadi ya watu Nairobi ni takribani milioni saba, siwezi kusema nimechaguliwa Gavana nichukue vijana milioni moja niwaajiri."

Gavana Sonko akiwakilisha nchi za bara la Afrika katika mkutano huo amesema ndoto zake kwa mji wa Nairobi ni..

(Sauti ya Mike Sonko)

Kuhakikisha Nairobi inakuwa mji msafi Afrika kushindana na Kigali, kuhakikisha tunamaliza msongamano wa magari. Na pia changamoto kubwa inayotusumbua Nairobi ni takataka. Takataka zetu tunapeleka Dandora lakini nikaona hiyo si sawa na tukaiga mifano namna nchi nyingine zinavyofanya mathalani Sweden au hapa Marekani ambapo mitambo inabadilisha takataka kuwa nguvu ya umeme.