Ϲ

Somalia imepiga hatua lakini jitihada zaidi zahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake:De Clercq

Get monthly
e-newsletter

Somalia imepiga hatua lakini jitihada zaidi zahitajika kukomesha ukatili dhidi ya wanawake:De Clercq

UN News
By: 
Mama mmoja akiwa na watoto wake akiwa amekaa nje ya makazi yake ya muda nje ya mji wa Belet Weyne Somalia. Picha: UN Photo/Ilyas Ahmed
Picha: Patterson Siema. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa amataifa la wanawake-UN-Women,Phumzile Mlambo-Ngcuka,(kushoto) akiwa na wanawake wmjini Baidoa Somalia.
Picha: UN Photo/Ilyas Ahmed. Mama mmoja akiwa na watoto wake akiwa amekaa nje ya makazi yake ya muda nje ya mji wa Belet Weyne Somalia

Nchini Somalia leo kumezinduliwa kampeni ya siku 16 za uhamasishi kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa sekta zote za jamii nchini humo kuchukua hatua madhubuti kusaidia kukomesha ukatili huo.

Uzinduzi huo umefanyika mjini Mogadishu, na naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Peter de Clercq. Katika sherehe za uzinduzi huo bwana De Clercq amesema kuwa Somalia ,imepiga hatua katika kutoa adhabu na kukabiliana na makosa yanayohusiana na ukatili wa kingono na kijinsia.

Ameongeza kuwa katika ngazi ya shirikisho, baraza la mawaziri lilipitisha mswada mwezi Mei mwaka huu dhidi ya makoya ya ukatili wa kingono hatua ambayo amesema ni nzuri katika kukabiliana na ukatili na kuboresha msaada kwa waathirika wa ukatili huo.

Kampeni ya siku 16 ya uhamasishaji dhidi ya ukatili kwa wanawake , ni ya kimataifa na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

[[{"fid":"15537","view_mode":"default","fields":{"alt":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","title":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","class":"media-element file-default","data-delta":"1","format":"default","field_file_image_alt_text[und][0][value]":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","field_file_image_title_text[und][0][value]":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio"},"link_text":null,"type":"media","field_deltas":{"1":{"alt":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","title":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","class":"media-element file-default","data-delta":"1","format":"default","field_file_image_alt_text[und][0][value]":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","field_file_image_title_text[und][0][value]":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio"}},"attributes":{"alt":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","title":"Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawake wakiathimisha siku ya Wanawake Diniani 2018. Picha na UN/Hervé Serefio","class":"media-element file-default","data-delta":"1"}}]]

Kampeni hii inaanza leo Novemba 25, katika siku ya kimataifa ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na itaendelea hadi Disemba 10, wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mgogoro nchini Somalia, umedumaza maendeleo ya wanawake mfano kati ya watu milioni 4.2 wanaohitaji msaada wa kibinadamu karibu nusu yao ni wanawake. Isitoshe wahudumu wa misaada ya kibinadamu wakadiria kuwa watu milioni 2.6 ni wakimbizi wa ndani na wanawake na wasichana katika jamii zisizo na makazi wako hatarini ya kunyanyasiwa kijinsia wanakoishi.

Utafiti nchini Somalia unaonyesha kuwa unyanyasaji wa kutumia mabavu bado unashika nafasi ya kwanza nchini humo ukifuatiwa na ukatili wa kingono na ubakaji ambao unachukua asilimia 64 ya kesi zote zinazoripotiwa.

Bw. De Clercq amesema ukatili kama unyanyasaji wa kingono na kijinsia ni moja wa visa vinavyojitokeza sana wakati wa migogoro na vita nchini Somalia, na ametoa wito kwa kwa serikali ya shirikisho ya Somalia, serikali za majimbo na kwa wadau wote wa kitaifa na kimataifa kutoa mchango wao katika kuhamasisha, msaada wa kisheria na kimatibabu kwa wale ambao wako hatarini.

Mada: