Ϲ

Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imenisadia silali njaa -Fundi Beatrice

Get monthly
e-newsletter

Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imenisadia silali njaa -Fundi Beatrice

UN News
29 May 2020
By: 
Jamii inajitolea kutengeneza barakoa kwa wafanyakazi wa huduma za Afya huko Cox's Bazar Bagladesh
IOM
Jamii inajitolea kutengeneza barakoa kwa wafanyakazi wa huduma za Afya huko Cox's Bazar Bagladesh

Mlipuko wa virusi vya Corona aukwa kiasi kikubwa umeathiri kila nyanja ya maisha ya watu duniani kote ukiacha kwamba umesababisha mamilioni ya vifo lakini pia umeathiri uchumi na maisha ya kijamii.

Na athari hizo za kijamii ni pamoja na watu kupoteza pato la familia kutokana na kukpoteza ajira, watoto kushindwa kuhudhuria masomo na hata shughuli za ujasiriliamali kusambaratika hali ambayo imewafanya wengi kujikuta katika wakati mgumu kumudu maisha ya kila siku.

Lakini si kwa mjasiriliamali wa ufundi cherahani Beatrice Mbugi kutoka Mbeya Tanzania aliyeanza kazi hiyo ya ushoni tangu mwaka 1998, janga hili la corona limempa mwelekeo mpya wa kazi yake ya ujasirilamali.

Jina langu ni Beatrice Teso Mbugi, fundi wa kushona ninaishi kata ya Nzove Mbeya Tanzania.Hii kazi naipenda sana na nimejifunza mwaka wa 1998 lakini kwa kipindi hiki sasa cha huu ugonjwa ulioingia cha ukweli ni kwamba imekuwa ni changamoto kwa wateja wetu ambao wanashona nguo kwa vile hawaji na hawawezi kusema wanunue vitenge au vitambaa waje washone kwangu nguo. Ila wanajifungia ndani na kuwaza namna gani watajikinga na ugonjwa huu wa corona.

Hivyo basi nami kama fundi nimetumia fursa hii na kujiongeza, nimejiongeza nashona barakoa za kutosha. Hizi barakoa ni za kitambaa ambazo unaweza kuzitumia, ukafua vizuri na kuzinyosha vizuri tofauti na zile ambazo zinavaliwa masaa manne .

Sasa hiki kitambaa kinachotumika ni kitambaa cha pamba au cotton ni kizuri zaidi na tunaweka vitambaa pande mbili ambazo hata ukiongea haiwezi ikaloa.
Je Barakoa hizo anazozishina zinazingatia viwango na wananchi kuweza kuzimudu?
Hizi barakoa ninazishona za viwango tofautitofauti za shilingi elfu moja na elfu mbili kutokana na vile wateja wangu wanavyozihitaji. Wateja wangu wakubwa sana ni watu wa kwenye daladala, wapita njia wa rika kuanzia umri wa miaka kumi na nne na kuendelea pia kwa akina bibi pia tunawauzia hizi barakoa .Kwa kiwango hiki hapa ni shilingi elfu moja. Sishoni kama zile zingine zinashonwa tu kitambaa kimoja tu ili tu mtu avae, hizi zina kiwango angalau tumeweka kitambaa cha kwanza cha pili lakini pia ina mikanda hii ni shilingi elfu moja. Nayo hii ambayo iko tofauti kidogo hata ukiitazama ni nzito na ina mikandi miwili ya kupishana hapa.

Nilifika katika hospitali ya rufaa Mbeya nilifika pale na kukuta kweli wajasiriamali wameshona barakoa nyingi na kwa kweli mtu anakuwa na shida ya kuingia hospitalini na kuhudumiwa basi inabidi tu achukue lakini mimi niliangalia kiwango cha zile barakoa tunazoletewa za misaada nikaangalia mfumo na muundo wa ile barakoa nikaona nitengeneze ya kitambaa lakini pia nitengeneze ya sponji kama hii ambayo inaendana kabisa na ile kama ya msaada.

Pamoja na kuleta adhaCOVID-19pia imenisadia silali njaa:Fundi Beatrice

Ni muhimu sana kwa wananchi kutumia na pia zinanipatia mahitaji mazuri na nyumbani kwangu watoto hawalali njaa,kwa siku naweza nikashona barakoa zaidi ya hata ishirini. Changamoto zipo haziwezi zikakosekana unaweza ukakata kitambaa ukasema kwamba kwa vile jana niliuza sana ngoja leo niongezee mita za kutosha ili nishone ndio niuze sana,utashangaa siku hiyo ndio hujauza kabisaa.Hizo ndizo changamoto.