Ϲ

Nchi 170 zaidhinisha ombi la usitishaji uhasama wakati wa janga la COVID-19 -UN

Get monthly
e-newsletter

Nchi 170 zaidhinisha ombi la usitishaji uhasama wakati wa janga la COVID-19 -UN

UN News
25 June 2020
By: 
Watoto wakimbizi katika kambi za Zaatari nchini Jordan wakionyesha ishara ya amani
UN Photo/Sahem Rababah
Watoto wakimbizi katika kambi za Zaatari nchini Jordan wakionyesha ishara ya amani

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, nchi waangalizi na wengineo wametuma ujumbe mzito wa kisiasa wiki hii kwa kutangaza kwamba sahihi 170 sasa zimeidhinisha wito wa Umoja wa Mataifa wa kunyamazisha silaha na kusimama Pamoja dhidi ya tishio la kimataifa la janga la virusi vya corona au COVID-19.

Mkakati huo ulioanzishwa na Malaysia sasa umeonyesha kwamba idadi kubwa ya nchi hii sasa zinasimama bega kwa bega na wito wa kimataifa wa usitishaji vita uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Machi wakati janga la COVID-19 ndio lilikuwa likishika kasi.

Taarifa iliyotolewa Jumanne imeelezea wasiwasi mkubwa kwa maeneo ya dunia ambako mapigano yanaendelea hususan katikati ya mgogoro mkubwa wa kiafya duniani.

Huku ikiainisha athari kwa walio hatarini zaidi hususan wanawake na Watoto taarifa hiyo imesema“Ni lazima tushike usukani wa juhudi zetu ili kuokoa maisha na kupunguza athari za kiuchumi na kijamii kwa watu wetu.”

Kuchukua hatua za pamoja

Nchi zilizoyia saini zimesisitizakwamba hatua za kidplomasia na juhudi za pamoja zinahitajika katika vita vya pamoja dhidi ya COVID-19 na kuhimiza umuhimu wa umoja na mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na jinamizi la corona.”

Katikati ya athari za janga hili la corona katika nguzo zote tatu za Umoja wa Mataifa ambazo ni amani na usalama, maendeleo na haki za binadamu, mataifa yamesisitiza umuhimu wa umoja wa kimataifa, utawala wa sharia, diplomasia na majadiliano kama msingi wa kuchagiza na kusaidia utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani.

“Tunazingatia kwamba mazingitra ya amani hayana mpinzani katika kuwezesha fursa za kibinadamu katika maeneo tete na yaliyoathirika na vita.”

Taarifa hiyo imeeleza kinagaubaga ikiamini kwamba “juhudi za kupunguz madhila kwa binadamu na suluhu ya migogoro vinapaswa kwenda sanjari katika kuongoza hatua za kushughulikia janga la COVID-19.”

Tuipe amani fursa

Katika kuelekea maadhimisho ya 75 ya kutiwa Saini kwa katika ya Umoja wa Mataifa mnamo Juni 26 mwaka 1946, watia Saini hao kutoa nchi wanachama wametoa wito kwa pande zote katika mizozo kufanya kila waawzalo kutekeleza witio wa usitishaji uhasama.

Wamesema“Tuko pamoja katika utu wetu wa Pamoja na katika kuipa amani fursa.”

Mshikamano wa Pamoja

Kwa kufuata mtiririko wa alfabeti ifuatayo ni orodha kamili ya nchi zilizotia Saini na kuidhinisha wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa usitishaji uhasama hadi sasa.

Afghanistan, Albania, Algeria, Andorra, Angola, Antigua and Barbuda, Argentina, Armenia, Australia, Austria, Bahamas, Bahrain, Bangladesh, Barbados, Belarus, Belgium, Belize, Benin, Bhutan, Bolivia, Bosnia and Herzegovina, Botswana, Brazil, Brunei Darussalam, Bulgaria, Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Canada, Central African Republic, Chile, China, Colombia, Comoros, Costa Rica, Côte D'ivoire, Croatia, Cyprus, Czech Republic, Denmark, Djibouti, Dominica, Dominican Republic, Ecuador, Egypt, El Salvador, Equatorial Guinea, Eritrea, Estonia, Eswatini, Ethiopia, Fiji, Finland, France, Gambia, Georgia, Germany, Ghana, Greece, Grenada, Guatemala, Guinea, Guyana, Haiti, Honduras, Hungary, Iceland, Indonesia, Iraq, Ireland, Italy, Jamaica, Japan, Jordan, Kazakhstan, Kenya, Korea, Laos, Latvia, Lebanon, Lesotho, Liberia, Libya, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg, Madagascar, Malawi, Malaysia, Maldives, Mali, Malta, Marshall Islands, Macedonia, Mauritania, Mauritius, Mexico, Micronesia, Moldova, Monaco, Mongolia, Montenegro, Morocco, Mozambique, Namibia, Nepal, Netherlands, New Zealand, Niger,Nigeria, Norway, Oman, Palau, Palestine, Panama, Paraguay, Peru, Philippines, Poland, Portugal, Qatar, Romania, Rwanda, Saint Kitts and Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Samoa, San Marino, Sao Tome and Principe, Saudi Arabia, Senegal, Serbia, Seychelles, Sierra Leone, Singapore, Slovakia, Slovenia, South Africa, South Sudan, Spain, Sri Lanka, Sudan, Suriname, Sweden, Switzerland, Tajikistan, Tanzania, Thailand, Timor-Leste, Togo, Tonga, Trinidad and Tobago, Tunisia, Turkey, Turkmenistan, Tuvalu, Uganda, Ukraine, United Arab Emirates, United Kingdom, Uruguay, Uzbekistan, Vanuatu, Venezuela, Viet Nam, Yemen, Zambia, Zimbabwe and the European Union.