Ϲ

Mwanamke kuchagua kazi ni kujibagua -Sajini Bari Mwita

Get monthly
e-newsletter

Mwanamke kuchagua kazi ni kujibagua -Sajini Bari Mwita

UN News
1 June 2020
By: 
Sajini Bari Mwita, mwanamke pekee dereva na fundi makenika katika kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, huko Beni, DRC akijiandaa kurekebisha gari lililoharibika.
TANZBATT 7 Video
Sajini Bari Mwita, mwanamke pekee dereva na fundi makenika katika kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, huko Beni, DRC akijiandaa kurekebisha gari lililoharibika.

Sajini Baru Mwita ambaye ni dereva na fundi pekee mwanamke kutoka Tanzania akihudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, amesema kitendo cha mwanamke kuchagua kazi ni kujibagua yeye mweyewe.

Mlinda amani huyo katika kikundi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi cha, FIB amesema hayo akiwa huko Beni, Mavivi jimboni Kivu Kaskazini akifafanua kuwanawashauri wanawake waingie kwenye fani hii kwa sababu ni rahisi. Ni moyo wa kujitoa kufanya kazi hii kwa sababu kuna uzito wa baadhi ya mambo, kubeba vifaa, lakini kwa fani ya kijeshi nadhani ni rahisi sana kwa sababu unachangamana na watu wengi, napata ujuzi kutoka kwa watu mbali mbali. Kikubwa ninachoshauri wanawake wenzangu tusiangalie kazi, kwa mwanamke ukiangalia kazi unakuwa unajibagua. Tumeomba 50 kwa 50 mimi naomba iwe 100 kwa 100. Kama tunafanya kazi ni kusonga mbele, basi tunasonga mbele.”

Sajini Bari ambaye ambaye alikuwa na vifaa vya kiufundi mkononi akaulizwa alichokuwa anafanya akasema kuwa,« nilikuwa narekebisha gari lililotoka Matembo lilikuja limeharibika. Kwa hiyo nilikuwa narekebisha baadhi ya vifaa na kukaza boriti zilizokuwa zimelegea. Jukumu kubwa la magari yetu ni kusafirisha walinda amani kutoka sehemu moja au nyingine. Au kama kuna ghasia zimetokea mahali tunajipanga tunakwenda. Tunakwenda na magari ya kubeba askari au hata vifaru. Tofauti pia ni kwamba siyo tu ni fundi bali pia nina uwezo wa kuyaendesha. Magari ninayoendesha ni pamoja na malori, magari ya kunyanyua mizigo na hata magari makubwa ya mizigo.”

Kuhusu changamoto anazokumbana nazo, Sajini Bari amesema ni barabara kwa sababu,“tumeshazoea kuendeshea upande wa kulia na hizi ni upande wa kushoto, kwa hiyo unakutana na jukumu kubwa, lakini kwa sababu napenda hii kazi, yote najifunza kwa siku moja na natekeleza kulingana na majukumu."