爆料公社

Mnamo Siku ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza mshikamano katika vita dhidi ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Mnamo Siku ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza mshikamano katika vita dhidi ya COVID-19

Secretary-General Ant贸nio Guterres
Afrika Upya: 
25 May 2020
Secretary-General Ant贸nio Guterres
Secretary-General Ant贸nio Guterres

Mwaka huu ulimwengu unaadhimisha Siku ya Afrika katika hali ngumu sana tunapokabiliana na janga la kimataifa la COVID-19, linalotishia kulemaza maendeleo ya mataifa ya Afrika kuelekea kumitiza Malengo ya Maendeleo Endelevu na malengo yaliyowekwa katika Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

Mataifa ya Afrika yemedhihirisha uongozi bora kupitia mapambano ya haraka na yaliyoratibishwa. Umoja wa Afrika uliunda jopokazi kuweka mkakati wa kibara na kuteua mabalozi maalumu kutafuta usaidizi wa kimataifa. Baraza lake la Usalama pia limechukua hatua kupambana na athari hasi za COVID-19 katika utekelezaji wa makubaliano muhimu ya amani na juhudi za mapatano. Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa vya Afrika vilianzisha hazina za mapambano, huku Mataifa Wanachama wa Afrika yakitekeleza hatua madhubuti ya kudhibiti kuenea kwa virusi na kuzuia athari kwa jamii na uchumi.

Nafurahia kuungwa mkono na Umoja wa Afrika katika wito wangu wa kimataifa wa kusitisha vita ili tuangazie janga la COVID-19 - umuhimu ambao pia unaakisi kauli mbiu ya 2020 ya Umoja wa Afrika: ''Kuacha silaha: Kuunda mazingira bora kwa Maendeleo ya Afrika.'' Makundi yaliyo na silaha huko Kameroon, Sudan na Sudan Kusini wameitikia wito huo na kutangaza kuacha silaha kwa umoja. Ninasihi makundi mengine yaliyo na silaha na serikali za Afrika zifanye vivyo hivyo. Ninakaribisha pia uungwaji mkono wa nchi za Afrika kwa wito wangu wa amani nyumbani, na kukomesha aina zote za dhuluma, ikiwemo dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana.

Karibu nchi 20 za Afrika zimepanga kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu, chaguzi zingine zitaahirishwa kwa sababu ya janga hili, na kuna uwezekano wa kutatiza utulivu na amani. Ninawasihi wahusika wa kisiasa wa Afrika kushiriki katika mjadala jumuishi endelevu wa kisiasa ili kupunguza mvutano kuhusu uchaguzi na kushikilia vitendo vya demokrasia.

Umoja wa Mataifa umetoa muhtasari wa sera unaoelezea athari za janga hili barani Afrika. Tunatoa wito wa kupunguziwa deni na hatua ya kudumisha bidhaa za chakula, kulinda kazi na kuokoa bara dhidi ya kupoteza mapato na kusafirisha mapato nje. Nchi za Afrika, kama kila mtu, kila mahali, zinapaswa pia kuwa na upatikanaji wa haraka, sawa na kwa

bei nafuu wa chanjo yoyote na matibabu. Serikali za Afrika, kama zile nyingine zote ulimwenguni, zinaweza kutumia wakati huu kuunda sera mpya ambazo zitasaidia mifumo ya afya, kuboresha ulinzi wa kijamii na kufuata njia bora kwa tabianchi. Kulenga hatua kwa wale walioajiriwa katika sekta isiyo rasmi, ambao wengi wao ni wanawake, litakuwa jambo muhimu la kupona, kama itakavyo kwa ushiriki kamili wa wanawake na uongozi. Ushirikishwaji na uongozi wa vijana pia utakuwa muhimu katika kila hatua.

Katika Siku ya Afrika hii, ninathibitisha tena kushikana kwangu kikamilifu na watu na Serikali za Afrika katika kupambana na janga la COVID-19 na kuunda njia ya maendeleo kamili baada ya janga na mustakabali bora kwa wote.