Ϲ

Kuwekeza katika kuikinga jamii ni muhimu ili bara la Afrika liweze kujijenga baada ya COVID-19

Get monthly
e-newsletter

Kuwekeza katika kuikinga jamii ni muhimu ili bara la Afrika liweze kujijenga baada ya COVID-19

Kutoa pesa na chakula kunaweza kupunguza unyonge wa watu na kuimarisha usawa
Afrika Upya: 
24 March 2021
Investing in social protection critical for Africa to build back better after COVID-19
Kuwekeza katika kuikinga jamii ni muhimu ili bara la Afrika liweze kujijenga baada ya COVID-19.

Japokuwa Afrika imeshuhudia visa na vifo vichache vya COVID-19 ikilinganishwa na mabara mengine, raia wake wameathirika zaidi na athari za kiuchumi na kijamii zilizotokana na janga hili.

Mataifa ya Afrika yanashuhudia hali isiyo ya kawaida ya kudorora kwa uchumi ambayo imehujumu utekelezwaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu.

Bara hili limeingia katika udororaji wa uchumi kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25, na ukuaji wa mapato ya nchi kwa mwaka 2020 umeshuka kwa asiliamia 1.6. Kusini mwa jangwa la Sahara, ukuaji ulikisiwa kushuka kwa asilimia 3.3 mwaka 2020, na kusitisha ukuaji ambao umekuwa kwa mwongo mmoja.

Mikakati ya kufunga nchi na kudorora kwa uchumi ni visababishi vya ukosefu wa ajira, umaskini, ukosefu wa chakuka na ukosefu wa usawa.

Nafasi za ajira milioni 60 zilizopotea Afrika

Takriban kazi milioni 60 za kudumu zilipotezwa katika robo ya pili ya mwaka 2020 barani Afrika, zikiwemo nafasi milioni 45 katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Watu milioni 40 waliingia katika umaskini mkubwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2020 Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Serikali zimechukua hatua nyingi za kijamii kukabiliana na janga la COVID-19

Ili kukabiliana na janga hili, serikali za Afrika zimeingilia kati kwa kuweka mikakati ya sera na mipango ya kijamii zaidi ya mia mbili yenye lengo la kupunguza umaskini na Mazingira hatarishi.

Hatua zilizochukuliwa na serikali za Afrika zinahusisha sana fedha ama chakula kilichotolewa kwa watu au biashara ndogondogo ambazo mapato yake yameathiriwa sana na janga hili.

Hatua nyingine za sahali ni pamoja na kuwaruhusu watu kuahirisha ulipaji wa bili za maji na umeme, kusaidia ulipaji wa bili hizo, na pia kulipa mishahara ya wafanyakazi wa kampuni binafsi iwapo waajiri wao watashindwa kufanya hivyo.

Hatua hizi zinapunguza kudhalilika kwa watu kutokana na athari za kiuchumi na kijamii, na pia kuboresha uwezo wao wa kumudu athari kama vile ukosefu wa ajira, kutengwa, maradhi, ulemavu na ukongwe. Ulinzi wa kijamii unaboresha usawa.

Nchi nyingi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara zimeanzisha mikakati mipya au kuboresha mikakati iliopo ili kufikia idadi kubwa zaidi ya waathirika.

Kuwekeza zaidi kwa ajili ya ulinzi wa jamii ni muhimu katika kuyasaidia mataifa ya Afrika kurudi katika hali yao ya awali.

Japokuwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali za Afrika zilikua ni za muda mfupi, zimeonyesha uwezo wa kustahimili ambao ulizi wa jamii unaweza kusaidia.

Kuendelea mbele, nchi za Afrika zinapaswa kujijenga kupitia hatua hizi za muda mfupi ili ziwe za kudumu na kuimarisha mikakati ya muda mrefu ya ulinzi wa jamii.

Kuwekeza katika ulinzi wa jamii ni muhimu katika kusaidia mataifa ya Afrika kujiimarisha tena, ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Wakati serikali zinaweza kutumia rasilimali zao za ndani kama vile ushuru na michango ya hifadhi ya jamii, zinaweza pia kuongeza matumizi kwa ajili ya ulinzi wa jamii kupitia washirika wa maendeleo wa kimataifa na sekta mbali mbali za kikanda.

Wadau wa maendeleo wamehimizwa kusaidia juhudi hizi, hasa katika nchi masikini ambazo zina kipato kidogo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa António Guterres alisema ushirikiano wa kimataifa na Afrika ni muhimu – sasa na ili kurejea vizuri katika hali ya awali.

“Umoja wa Mataifa, na mimi binafsi, kwa mshikamano, tunasimama na watu pamoja na serikali za Afrika na Umoja wa Afrika katika kupambana na COVID-19,” Bwana. Guterres alisema.

Hatimaye, nchi zilenge kuwa na ulinzi wa jamii kwa wote kupitia sera za kitaifa na mipango inayolinda maisha yao dhidi ya umaskini na hatari kwa ustawi wa maisha yao ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

“Ulinzi wa jamii umesaidia sana katika kuzuia athari za kijamii-uchumi za janga la COVID-19 barani Afrika. Wakati nchi zake zikihangaika kujikwamua kutoka katika janga hili ambalo limeathiri zaidi maskini sana na wasio na uwezo, kuimarisha ulinzi wa jamii kutaongeza mtazamo wa kiusawa hapo baadaye. Bwa. Liu Zhenmin alisema, Katibu wa idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii (UN DESA).

“UN DESA imeongeza juhudi katika chaguzi za kisera ili kuisaidia Afika kurudi katika hali yake ya awali baada ya COVID-19 na duniani kote. Kadhalika, kuziwezesha nchi wanachama kutekeleza mifumo madhubuti ya ulinzi wa jamii kutasaidia kuleta njia yenye ustahimilivu na inayojumuisha watu wote ambayo inaendana na Ajenda ya mwaka 2030 na kutomuacha mtu nyuma”, aliongezea Mr. Zhenmin

Mapendekezo

Serikali ziangalie uwezekano wa kutumia teknolojia ya kidijitali (kama vile majukwaa ya fedha ya simu ambayo yanatumika sana Afrika) ili kutoa huduma kwa haraka na kwa usalama kwa njia ambayo inaheshimu faragaha ya mtu.

Serikali zinapaswa kuwalenga walio katika mazingira hatarishi, wakiwemo wanawake, wahamaji, wakimbizi na wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kupitia mipango iliyowekwa na mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kimataifa. Yanapaswa kuendelea kutafuta mbinu za ubunifu katika kutoa msaada kwa kijamii kupitia mashirika ya kijamii ambayo yanahimiza mabadiliko ya tabia ili kusaidia malengo ya afya ya umma.

  • Kwa taarifa zaidi, tazama mukhtasari wa Sera kwa Ufupi namba 93 ‘Sera ya jamii na hatua kwa ulinzi wa jamii ili kuiimarisha Afrika baada ya Covid-19” iliyotayarishwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha masuala ya Kiuchumi na Kijamii (DESA) /en/desa/policy-briefs.
  • Tazama waandishi - Hantamalala Rafalimanana and Meron Sherif walipokua wakitoa matokeo makuu na mapendekezo ya mukhtasari huu wakati wa majadiliano mubashara kupitia Facebook katika DESA UN mwendelezo wa “Let’s Talk” ().
More from this author